Yanga, Simba, Azam na KMKM wapata wapinzani CAF

Droo ya michuano ya CAF imepangwa jijini Dar es Salaam jana, ikiwapa mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga, mechi ya awali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Wiliete Benguela ya Angola, huku Simba ikipangwa na Gaborone United ya Botswana.

Timu zote zitaanzia ugenini kati ya Septemba 19–21 na kurudiana Dar es Salaam Septemba 26–28.

Iwapo Yanga itasonga mbele, itakutana na mshindi kati ya Elgeco Plus (Madagascar) na Silver Striker (Malawi), na Simba itakutana na mshindi kati ya Simba Bhora (Zimbabwe) na Nsingizini Hotspurs (Eswatini).

Katika Kombe la Shirikisho, Azam FC itavaana na El Meriekh Bentiu ya Sudan Kusini, Singida Black Stars na Rayon Sports ya Rwanda, huku KMKM ya Zanzibar ikicheza na AS Port ya Djibouti.

Timu zote za Tanzania zitaanza hatua hiyo ugenini.

Meneja wa Yanga, Walter Harrison, amemsifu kocha mpya Romain Folz kwa kuunganisha wachezaji kwa muda mfupi na kutabiri mafanikio makubwa msimu ujao.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *