Klabu ya Yanga imekamilisha taratibu zote za kumsajili kiungo Ramadhan Salum Chobwedo, kufuatia mazungumzo yaliyoanza wiki iliyopita.
Taarifa zinaeleza kuwa Yanga walianzisha mazungumzo na mchezaji huyo mara baada ya mchezo dhidi ya Simba SC, huku mchakato wa kumtazama ukifanywa na baadhi ya wajumbe wa kamati ya usajili ya klabu hiyo.
Kutokana na uwezo wake uwanjani, Chombwedo anaonekana kuwa miongoni mwa wachezaji wanaoweza kuvutia mashabiki wa Yanga na Simba msimu huu wa ligi, bila kujali maisha yake nje ya uwanja.




