Yanga imemsajili beki wa kati, Frank Assinki raia wa Ghana, kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Singida Black Stars.

Assinki amejiunga na kambi ya Yanga na tayari ameanza mazoezi. Ofisa Habari, Ali Kamwe, amethibitisha kuwasili kwa mchezaji mpya lakini akasema jina litatajwa rasmi muda wowote.
Aidha, Kamwe ametangaza kuwa Yanga imerejea kambini Avic Town, Kigamboni baada ya ukarabati na kufichua kuwa Wiki ya Wananchi itafanyika Septemba 12, Uwanja wa Benjamin Mkapa sambamba na uzinduzi wa jezi mpya.




