Yanga yamwagiwa bilioni 3.3 kwa udhamini mpya

Klabu ya Yanga imeingia mkataba mpya wa udhamini wa miaka mitatu na kampuni ya Haier wenye thamani ya Shilingi bilioni 3.3.

Rais wa klabu hiyo, Hersi Said, alisema udhamini huo utaongeza chachu ya mafanikio, ikiwemo usajili wa wachezaji bora na maandalizi ya msimu ujao.

Hersi alisema mkataba wa awali ulisaidia kuifikisha Yanga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa. Aliahidi kuendeleza ushirikiano na Haier kwa maslahi ya klabu.

Meneja wa Haier, Ibrahim Kiongozi, alisema wameamua kuongeza mkataba kutokana na mafanikio makubwa ya Yanga, na wanaamini ushirikiano huu utaongeza zaidi mafanikio hayo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *