Zanzibar kuandika historia ya CHAN leo

Fainali za CHAN zinatarajiwa kuandika historia leo visiwani Zanzibar kwa mara ya kwanza, wakati Kundi D litakapoanza mechi zake kwenye Uwanja wa New Amaan Complex.

Mchezo wa kwanza utakuwa kati ya Congo Brazaville dhidi ya Guinea saa 11:00 jioni, ukifuatiwa na Senegal dhidi ya Nigeria saa 2:00 usiku.

Katibu Mkuu wa ZFF, Hussein Vuai, amesema maandalizi yamekamilika na hii ni fursa ya kipekee kwa Zanzibar. CHAN ya mwaka huu inashirikisha timu 19 zilizogawanywa katika makundi manne yanayochezwa Kenya, Uganda, Dar es Salaam na Zanzibar.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *