Tuesday, March 3, 2026
spot_img
HomeMichezo🟢 Gamondi Asema: Kuwait si ya kushinda, ni ya kujifunza

🟢 Gamondi Asema: Kuwait si ya kushinda, ni ya kujifunza

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imetua salama nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Kuwait, utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Al Salaam jijini Cairo.

Kaimu Kocha Mkuu wa Stars, Miguel Gamondi, amesema lengo la mchezo huo si ushindi, bali ni kuibua mapungufu na kuboresha kikosi kuelekea Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika baadaye mwaka huu nchini Morocco.

“Jambo muhimu kwangu si matokeo, bali kuwatazama na kuwatathmini wachezaji ili nijue maeneo gani yanahitaji maboresho,” alisema Gamondi kabla ya kuondoka nchini.

Stars, ambayo inashika nafasi ya 107 kwenye viwango vya FIFA, itakabiliana na Kuwait inayoshika nafasi ya 135 duniani. Kocha huyo alisema anataka kuona namna wachezaji wa klabu kama Simba na Yanga wanavyocheza, pamoja na kuwapa nafasi wachezaji wanaofanya vizuri kwenye Ligi Kuu Bara ili kupata kikosi cha mwisho kitakachoshiriki AFCON.

Gamondi, ambaye pia anakinoa kikosi cha Singida Black Stars, alisema anajisikia fahari kubwa kupata nafasi ya kuifundisha Taifa Stars na kuahidi kuunda kikosi imara kitakachoiwakilisha vyema Tanzania barani Afrika.

“Wachezaji wako na morali kubwa kambini, nami nina furaha. Tutajitahidi kuhakikisha tunatengeneza kikosi bora na madhubuti,” alisema.

Mara ya mwisho Taifa Stars ilicheza mechi ya kirafiki ya kimataifa Oktoba 15, mwaka huu, dhidi ya Iran huko Dubai, na kupoteza kwa mabao 2–0.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments