Tuesday, February 17, 2026
spot_img
HomeElimuVodacom yaongeza udhamini wanafunzi 1,000

Vodacom yaongeza udhamini wanafunzi 1,000

Kampuni ya Simu Vodacom Tanzania imeahidi kufadhili jumla ya vijana 1,000 kila mwaka katika Kituo cha Mafunzo ya Ufundi (VTC) cha Don Bosco ikiwa ni sehemu ya kuendeleza ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili.

Pia lengo ni fursa kwa vijana ili kujiongezea ufanisi katika soko la ajira au kuweza kujiajiri kwani dunia ya sasa inahitaji ujuzi, ubunifu na uthubutu.

Mkurugenzi wa Biashara na Masoko (CBU) Vodacom, Brigita Stephen akiekeza hayo wiki iliyopita Dar es salaam kwa niaba ya kampuni hiyo katika hafla ya mahafali ya wanafunzi wa Don Bosco VTC.

Akizungumza katika hafla hiyo Brigita alisema inatia moyo kuona vijana hao123 wamehitimu na wengi wao wameshapata kazi hali inayoonesha kuna fursa za ajira na hiyo ni ushahidi tosha kwamba mahitaji ya ujuzi wa ufundi nchini bado ni makubwa na soko la ajira.

“Wahitimu hawa wamefika safari moja ya maisha na kuanza nyingine, na wengi wao wameshapata kazi hii inaonesha kuna fursa ya ajira na huu ni ushahidi tosha kabisa na kwamba mahitaji ya ujuzi wa ufundi nchini bado ni makubwa, soko la ajira na upatikanaji wa mafunzi bado ni mkubwa,” alisema Brigita.

Aliongeza wao kama kampuni waliangalia hili tatizo wakasema kwamba wanatangaza rasmi dhamira yao ya kuongeza ushirikiano na Don Bosco nchini Tanzania na kuzindua rasmi ahadi yao ya kudhamini wanafunzi 1,000 kila mwaka.

Alisema katika ushirikiano walioingia mwanzo waliahidi kudhamini wanafunzi 50 kila mwaka lakini wakaona ni vyema kufadhili wanafunzi 1,000 na kuwezekeza katika vijana hao ili kuweza kuwaunga mkono katika safari yao ya teknolojia, elimu na fursa.

Katika hatua nyingine, alisema awali waliunda jukwaa maalumu la vijana wenye umri kuanza umri wa miaka 15 hadi 28 lililoitwa ‘Vodacom Youth Base’ (VYB) Ili kuhakikisha hakuna kijana anayeachwa nyuma katika uchumi unaoongozwa na maarifa na teknolojia.

Pia Brigita alisema wamechagua kushirikiana na kituo hiko kwa sababu ni taasisi inayoelelezi kile wao wanachokiamini kupitia mafunzo ya ufundi ujasiliamali, michezo na malezi ya maadili na ndiyo kitu muhimu kwao.

“Don Bosco imekuwa nguzo muhimu sana ya maandalizi ya vijana ya maisha na kazi nah ii inaendana moja kwa moja na ajenda yetu sisi ya kuwezesha bijana kwa ujuzi, fursa na dira ya maisha,” alisema Brigita.

Aliongeza ushirikiano wao haukuishia darasani bali pia kuwekeza katika michezo ikiwemo ukarabati wa uwanja wa mpira wa kikapu kwa sababu wanaamini michezo ni sehemu muhimu ya malezi, nidhamu na uongozi kwa vijana.

Mmoja wa wanufaika wa ufadhili huo, John Ottoman alisema yeye amesoma kozi ndefu ya umeme kwa muda wa miaka mitatu katika kituo hicho na ufadhili wa huo umemsaidia kutimiza ndoto yake kimasomo kwani mzazi wake hakuwa na uwezo wa kumlipia ada.

“kozo hii kwangu inafaida kwa sababu itanisaidia kujiendeleza kiuchumi, na ufadhili wa huu umetusaidia hata sisi ambao familia zetu kipato cha chini imenisaidia kulipa sehemu ya ada yangu, na nipo tayari kuendelea kusoma ili nije kujiajiri mwenyewe na kusaidia jamii yangu,” alisema Ottoman.

Mariam Msunu alisema ushiriki wa Vodacom umekuwa sehemu ya mafanikio kwao kwani wamepata nafasi ya kusoma na kunufaika na fursa hiyo japo bado anatamani kuendelea kusoma.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments