Kikosi cha Singida Black Stars kinatarajia kuondoka nchini Oktoba 17 kuelekea Burundi kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) dhidi ya Flambeau du Centre, utakaochezwa Oktoba 19.
Ofisa Habari wa klabu hiyo, Hussein Massanza, amesema maandalizi yanaendelea vizuri na wachezaji wako kwenye morali kubwa wakilenga ushindi ugenini.
“Kila mchezo kwetu ni kama fainali. Tunataka kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania,” alisema.
Timu hiyo itacheza mechi mbili za kirafiki kabla ya safari, ikijiweka tayari kwa mapambano makali barani Afrika.
Mbali na Singida BS, Tanzania Bara inawakilishwa pia na Azam FC, huku Simba SC na Yanga SC wakiwania taji la Ligi ya Mabingwa Afrika.





