Tuesday, March 3, 2026
spot_img
HomeMichezoSimba SC yazindua jezi mpya kutumika Ligi ya Mabingwa Afrika

Simba SC yazindua jezi mpya kutumika Ligi ya Mabingwa Afrika

Klabu ya Simba SC imezindua rasmi jezi zake maalum zitakazotumika katika hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Jezi hizo zinajumuisha rangi nyekundu ya jadi itakayotumika kama jezi ya nyumbani pamoja na jezi ya bluu ambayo ni jezi ya tatu au ya ziada.

Kwa sasa, Simba SC inatarajia pia kuwatambulisha jezi mpya ya ugenini yenye rangi nyeupe, ambayo itakuwa chaguo la tatu kwa wakati wowote utakaoona inafaa. Hii ni hatua ya kuonesha utofauti na pia kuleta msisimko na mvuto zaidi kwa mashabiki wa klabu hiyo.

Simba SC inatarajiwa kuanza safari yake katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Petro de Luanda kutoka Angola. Mechi hiyo itachezwa Novemba 23, 2025, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo jijini Dar es Salaam, ambapo mashabiki wanatarajiwa kuunga mkono kwa wingi katika tukio hilo kubwa la mpira wa miguu.

Uzinduzi huu wa jezi mpya unalenga kuongeza ari na kuipa timu motisha zaidi katika michuano hii mikubwa, huku ikiwalenga wachezaji na mashabiki kujivunia rangi na jezi zinazowakilisha Simba SC kwenye dimba la Afrika.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments