Tuesday, March 3, 2026
spot_img
HomeElimuTIA Singida yafanya utafiti 13 na kuimarisha ushauri wa kitaalam kwa mwaka...

TIA Singida yafanya utafiti 13 na kuimarisha ushauri wa kitaalam kwa mwaka 2024/2025

Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida imefanikiwa kufanya utafiti na machapisho 13 pamoja na kutoa ushauri wa kitaalam katika maeneo ya usimamizi wa fedha, biashara ndogo na za kati, na maendeleo ya jamii kwa mwaka wa masomo 2024/2025.

Utafiti huo umefanyika kwa lengo la kuchangia katika kutatua changamoto za kiuchumi na kijamii katika mkoa wa Singida na nchini kwa ujumla, huku ukilenga kuimarisha sekta ya ujasiriamali, kuongeza ufanisi wa usimamizi wa rasilimali fedha, na kuboresha ustawi wa jamii.

Akizungumza leo katika mahafali ya 23 ya TIA Kampasi ya Singida, Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA, Prof. William Pallangyo, alisema taasisi imeendelea kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya mkoa kupitia ushauri wa kitaalam kwa halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Singida pamoja na kutoa mafunzo ya muda mfupi kuhusu matumizi ya kompyuta.

Amesema katika mwaka huu wa masomo, Kampasi ya Singida imetoa wahitimu 1,490 na imeendelea kukua kwa kasi, ikichangia kuzalisha wataalam katika uhasibu, ununuzi na ugavi, biashara, rasilimali watu na masoko — maeneo muhimu katika utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 inayosisitiza kujenga jamii yenye elimu, ujuzi na uwezo wa kujifunza.

Prof. Pallangyo ameongeza kuwa, ili kuhakikisha utoaji wa elimu bora na yenye ufanisi unaoendana na mahitaji ya soko la ajira, TIA inaendelea kuboresha miundombinu ya kimkakati kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Kupitia mradi huo, Kampasi ya Singida imenufaika na Sh bilioni 13.5 kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya la kitaaluma.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments