Wednesday, December 10, 2025
spot_img
HomeMichezoTimu ya Taifa ya Wasichana U-15 yaandika historia Uganda

Timu ya Taifa ya Wasichana U-15 yaandika historia Uganda

Timu ya Taifa ya Wasichana U-15 ya Tanzania imeweka rekodi mpya baada ya kutwaa ubingwa wa Mashindano ya CAF African Schools Football Championships – CECAFA Qualifiers 2025 yaliyofanyika nchini Uganda.

Tanzania ilitwaa taji hilo kwa ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Ethiopia, katika mchezo mkali uliowakutanisha timu hizo mbili zilizong’ara zaidi katika hatua za awali. Matokeo hayo yameifanya Tanzania kuwa mabingwa wa ukanda wa CECAFA kwa mwaka 2025.

Ushindi huu unaibua sura mpya kwa taifa katika soka la shule, na kuitambulisha Tanzania kama moja ya nguvu mpya zinazochipukia katika mpira wa miguu wa wanawake katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments