Ligi ya Championship inaendelea kesho kwa pambano kali kati ya Songea United na Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea.
Ofisa Habari wa TPLB, Karim Boimanda, amesema wanasisitiza usimamizi makini ili ligi ipate mshindi wa haki.
Amesema ushindani wa msimu huu ni mkubwa na kila mechi imekuwa kama fainali.
Michezo mingine ya kesho:
- KenGold vs African Sports
- Stand United vs Transit Camp – Uwanja wa Mabatini
- Gunners vs Berberian – Morogoro
Keshokutwa:
- Geita Gold vs Mbuni – Arusha
- B19 vs Bigman
- Kagera Sugar vs TMA
- Hausung vs Mbeya Kwanza
Timu zitakazomaliza juu zitapanda daraja kucheza Ligi Kuu msimu wa 2026/27.




