Wednesday, December 10, 2025
spot_img
HomeMichezoSimba, Yanga zatimua makocha 16

Simba, Yanga zatimua makocha 16

Ni katika kipindi cha miaka mitano, huku wakifika fainali CAF mara moja…

Vigogo wa soka nchini, Simba na Yanga, wamepitia mikononi mwa makocha 16 ndani ya kipindi cha miaka mitano, Simba wakiwa na idadi kubwa zaidi ya tisa, huku Yanga wakiongozwa na saba.

Timu hizo zimekuwa zikibadilisha makocha mara kwa mara kutokana na presha ya kutaka ushindi wa haraka na mafanikio ya mara kwa mara. Wengi wameondolewa kwa kutofikia malengo, ingawa baadhi yao huondoka kwa “makubaliano ya pande mbili”.

Kwa upande wa Yanga, makocha waliopita ni:
Nasreddine Nabi (aliyefanya kazi kubwa kimataifa), Cedric Kaze, Miguel Gamondi, Saed Ramovic, Miluod Hamdi, Romain Folz na Pedro Goncalves anayeiongoza sasa.
Nabi ndiye aliweka msingi wa mafanikio ya kimataifa, akiiongoza Yanga mpaka fainali ya Kombe la Shirikisho CAF, ikipoteza kwa sheria ya mabao ya ugenini dhidi ya USM Alger.

Gamondi aliipeleka Yanga hadi robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka jana, ambako walitolewa na Mamelodi Sundowns kwa penalti.

Kwa upande wa Simba, waliowahi kukaa benchi la ufundi ni:
Sven Vandenbroeck, Didier Gomes, Pablo Franco, Zoran Maki, Juma Mgunda, Robertinho Oliveira, Abdelhak Benchikha, Fadlu Davids na Dimitar Pantev.
Waliowahi kufanya vizuri zaidi ni Sven, Didier Gomes, Pablo, Mgunda na Robertinho, waliowahi kuipeleka Simba hatua ya makundi, robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.

Kwa sasa, timu hizo zipo hatua ya makundi CAF.
Yanga ina pointi nne kwenye Kundi B baada ya kushinda mechi ya kwanza nyumbani na kutoka sare Algeria, huku Simba ikipoteza mechi zake mbili dhidi ya Petro de Luanda (1-0) na Stade Malien (1-0).

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments