Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatarajia kufanya uchaguzi mdogo mapema mwakani kujaza nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Kanda Namba 1, baada ya Hosea Lugano kujiuzulu.
Lugano alijiuzulu ili kuepuka mgongano wa maslahi wakati alipogombea uenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPLB), nafasi aliyoshindwa baada ya kupata kura sita, huku Nassor Idrissa wa Azam FC akiibuka mshindi.
Taarifa kutoka TFF zinaeleza kuwa uchaguzi huo utafanyika kwa mujibu wa katiba.
Inadaiwa kuwa Mwenyekiti wa DRFA, Lameck Nyambaya, anatarajiwa kutangaza nia — muda ukifika.
Kanda Namba 1 inajumuisha mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Lindi na Mtwara.




