Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameipatia tuzo Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa kutambua mchango wake na unaotolewa na Mamlaka hiyo katika usimamizi wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini.
Tuzo hiyo iliyotolewa wakati wa Usiku wa Tuzo za Umahiri katika Sekta ya Maji, jana Februari 23, Jijini Arusha, na kupokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dk. James Andilile.




Akizungumza baada ya kukabidhi tuzo hiyo, Aweso alieleza kuwa, lengo za tuzi hizo ni kutambua utendaji bora wa mamlaka za maji, wasimamizi na watendaji katika maeneo waliofanya vizuri kwa kipindi cha miaka mitatu (2021/22, 2022/23 na 2023/24).
Akizungumza baada ya kupokea tuzo, Dk. Andilile, alisema kuwa EWURA itaendelea kushirikiana na Wizara ya Maji pamoja na kuzisimamia kwa uthabiti ili ziendelee kufanya vizuri katika utoaji wa huduma.






