Straika mpya wa Yanga, Celestin Ecua, aliachwa kwenye kikosi cha Chad kilichocheza na Madagascar ili awahi kilele cha Tamasha la Wiki ya Mwananchi litakalofanyika keshokutwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Ecua alifunga bao la kusawazisha dhidi ya Ghana wiki iliyopita kwenye mechi ya kufuzu Kombe la Dunia kabla ya kuomba ruhusa kurejea nchini.
Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, alisema straika huyo ameamua kuwepo kwenye tamasha kubwa la kuwakutanisha mashabiki na wachezaji.
Aidha, alithibitisha kuwa mchezaji Clement Mzize pia atapanda jukwaani kuonesha kipaji chake cha uimbaji.
Tamasha hilo litakuwa la saba tangu lianzishwe mwaka 2019.




