Valentino Mashaka, mshambuliaji wa Simba aliyejiunga na JKT Tanzania kwa mkopo wa mwaka mmoja, ameanza rasmi mazoezi na kikosi chake kipya.
Usajili wake ni sehemu ya makubaliano ya Simba na JKT baada ya klabu hiyo ya maafande kuachia kipa Yakoub Suleiman na beki Wilson Nangu.
Mashaka alisema amefurahi kupata nafasi hiyo ili kuongeza muda wa kucheza na kujiweka kwenye rada ya timu ya taifa.




