JKT Tanzania imetambulisha rasmi wachezaji wapya kutoka Simba, Salehe Karabaka na Valentino Mashaka.
Ofisa Habari, Masau Bwire, amesema ujio wao unaipa timu jeuri ya kusajili popote na kutabiri wanaweza kuifikisha kimataifa.
Hata hivyo, wachezaji hao wamejiunga kwa mkopo wa mwaka mmoja.
Usajili huu ni sehemu ya makubaliano baada ya JKT kuwauzia Simba wachezaji Yakoub Suleiman na Wilson Nangu.




