Nyota wapya wa Simba SC, Rushine de Reuck na Neo Maema, wamesema wamestaajabishwa na umati wa mashabiki pamoja na shamrashamra za Simba Day, wakieleza kuwa uzoefu huo umewapa moyo wa kupambana msimu ujao.
Walisema tamasha hilo limeonesha ukubwa wa klabu hiyo na upendo wa mashabiki.
Katika kilele cha tamasha hilo, Simba iliifunga Gor Mahia ya Kenya mabao 2-0 kupitia Abdulrazaq Hamza na Stevin Mukwala.
Timu hiyo sasa inaelekeza nguvu kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga utakaopigwa Septemba 16, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.




