Thursday, December 18, 2025
spot_img
HomeMichezoDili la Mukwala Uarabuni lilivyokwama dakika za mwisho

Dili la Mukwala Uarabuni lilivyokwama dakika za mwisho

Nyota wa Simba SC, Steven Mukwala, ameendelea kuwa sehemu ya wachezaji 30 wa kikosi kipya cha Wekundu wa Msimbazi kwa msimu wa 2025/2026, licha ya awali kuhusishwa kwa karibu na kuondoka kwenda kucheza soka la kulipwa Uarabuni. Straika huyo raia wa Uganda alitajwa kuwa hatua ya mwisho ya kuuzwa, lakini dili hilo lilikwama dakika za mwisho kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili la Tanzania usiku wa Septemba 7.

Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na vigogo wa klabu moja kubwa ya Uarabuni, mipango ya kumsajili Mukwala ilikuwa imepigiwa hesabu zote, lakini ikaishia njiani. Mabosi hao walipozungumza na gazeti la Mwanaspoti walifichua kwa undani sababu zilizopelekea mpango huo kuvunjika.

Chanzo kilicho karibu na mazungumzo hayo kimeeleza kuwa siku moja kabla ya dirisha la usajili kufungwa, Al Ittihad ya Libya ilituma ofa nono mezani, ikitaka kumsajili mshambuliaji huyo hatari ambaye amebakisha mwaka mmoja kwenye mkataba wake na Simba. Ofa hiyo ilionekana kuvutia, na mazungumzo kati ya uongozi wa Simba na Al Ittihad yaliendelea kwa kasi kubwa, huku pande zote mbili zikikaribia kufikia makubaliano.

Hata hivyo, hadi kufikia Jumapili usiku wakati dirisha likifungwa rasmi, dili hilo lilikuwa bado halijakamilika. Vyanzo vya karibu na uhamisho huo vinaeleza kuwa tofauti ndogo za kifedha pamoja na masharti ya mkataba ndiyo yaliyopelekea mvutano, hali iliyosababisha mpango huo kuvunjika ghafla.

Kwa sasa, Mukwala ataendelea kubaki Msimbazi akihusiana moja kwa moja na jukumu la kutafuta mabao yatakayoisaidia Simba katika safari yao ya kusaka mataji ya ndani na ya kimataifa. Uwepo wake unaelezwa kuongeza nguvu kubwa kwenye safu ya ushambuliaji ya Wekundu wa Msimbazi, hasa ikizingatiwa namna alivyoonyesha makali yake msimu uliopita.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments