Friday, December 19, 2025
spot_img
HomeHabariMadereva wamshukuru Rais Samia kupata ajira Qatar

Madereva wamshukuru Rais Samia kupata ajira Qatar

Vijana wa Kitanzania waliopata ajira kama madereva nchini Qatar wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa jitihada zake kubwa za kufanikisha upatikanaji wa ajira stahiki nje ya nchi.

Mmoja wa vijana hao, John Kiango, alisema nafasi hizo zimekuwa suluhisho la changamoto za ajira na zitabadilisha maisha yao pamoja na familia zao.

“Kwanza kabisa, tunapenda kumshukuru Mama yetu, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, kwa jitihada zake kubwa za kuhakikisha vijana wa Kitanzania tunapata ajira nje ya nchi zinazostahiki.

Kupitia nafasi hizi, sisi vijana madereva tumepata ajira nchini Qatar, jambo litakalobadilisha maisha yetu na ya familia zetu.

Tunaahidi kufanya kazi kwa bidii, kwa nidhamu, na kuenzi heshima ya Tanzania kila tunapokuwa nje ya nchi,” alisema Kiango.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments