Friday, December 19, 2025
spot_img
HomeAfyaMNH,NHIF zajadili ushirikiano kuboresha huduma

MNH,NHIF zajadili ushirikiano kuboresha huduma

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Delilah Kimambo, amefanya kikao kazi na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dk. Irene Isaka, ikiwa ni sehemu ya kujitambulisha rasmi tangu kuteuliwa kwake kuongoza hospitali hiyo kubwa nchini.

Katika kikao hicho, viongozi hao wamejadili kwa kina namna ya kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili ili kuhakikisha wanachama wa NHIF wanapata huduma bora, za haraka na zenye ufanisi zaidi.

Miongoni mwa maeneo yaliyopewa kipaumbele ni kupunguza malalamiko ya wanachama, kuimarisha mifumo ya kielektroniki ya kutoa huduma, pamoja na kuongeza ubunifu katika utoaji wa huduma za afya ili kuendana na mahitaji ya jamii na mageuzi ya sekta ya afya nchini.

Dkt. Kimambo amesisitiza dhamira ya MNH kushirikiana kwa karibu na NHIF katika kuhakikisha wananchi, hususan wanachama wa mfuko huo, wanaendelea kupata huduma bora zinazostahili.

Kwa upande wake, Dkt. Isaka amepongeza ushirikiano unaoendelea kujengwa na Muhimbili, akibainisha kuwa NHIF itaendelea kuboresha mifumo yake na kushirikiana na hospitali hiyo ili kuondoa changamoto zinazowakabili wanachama wake.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments