Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Mwinyi amehimiza amani, umoja, mshikamano na maridhiano nchini Tanzania kwa kuwa ndicho kipaumbele cha chama hicho.
Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo, Jumatano Septemba 17, 2025 alipozungumza katika mkutano wa kampeni za Mgombea urais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, Makunduchi visiwani Zanzibar.




