“Tunaingia kipindi cha Uchaguzi, mwanzo nilipokuja kujitambulisha ahadi kubwa niliyoitoa ni kuifanya Tanzania iwe na amani na utulivu. Na nilipotembelea kisiwa cha Pemba, kubwa waliloniomba wazee kufanya uchaguzi kwa amani na utulivu na hili ndilo nalotaka kulitilia mkazo. Tunakwenda kwenye Uchaguzi mkuu, kwenye nchi yetu ninawaomba sana twende tudumishe amani na utulivu. Uchaguzi si vita, uchaguzi ni tendo la kidemokrasia ni watu kwenda kwa utaratibu uliowekwa”, Dkt. Samia Suluhu Hassan Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM).




