Straika wa KMC, Daruweshi Saliboko, aliibuka shujaa kwa kufunga bao pekee lililoipa timu yake ushindi wa 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu msimu huu.
Saliboko alifunga dakika ya 55 mara baada ya kuingia kutokea benchi, kufuatia maelekezo ya kocha wake kuhusu mianya ya wapinzani.
Bao hilo limempa heshima ya kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo, huku Dodoma Jiji ikiweka rekodi ya kuruhusu bao la ufunguzi wa msimu kwa mara ya pili mfululizo.






