Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan amesema chimbuko la elimu yake ya msingi ni visiwani Pemba, eneo ambalo Baba yake mzazi alikuwa anafanya kazi ya ualimu.
Sambamba na elimu ya msingi, amesema amewahi kuishi Pemba akiwa mfanyakazi baada ya kuhitimu elimu katika maeneo mbalimbali, kabla ya baadaye kuhamia mikoa mingine.
Dk. Samia ametoa kauli hiyo leo, Jumamosi Septemba 20, 2025 alipozungumza na wananchi wa Pemba visiwani Zanzibar, katika mkutano wake wa kampeni za urais.
“Mimi bwana ni Mpemba mwenzenu, Pemba oyeeeee…! Mara ya mwisho nilikuja Pemba kula futari na ndugu zangu, sasa mara hii nimekuja kwa shughuli maalumu ya kuomba kura,” amesema.




