Friday, December 12, 2025
spot_img
HomeBiasharaDk. Samia kujenga soko, mtambo wa samaki Nyasa

Dk. Samia kujenga soko, mtambo wa samaki Nyasa

Changamoto ya kukosa umeme wa uhakika wilayani Nyasa mkoani Ruvuma inakwenda kupata muarobaini, baada ya Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, kuahidi ujenzi wa kituo cha kupoza umeme katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa Dk. Samia, kituo hicho kitatokea wilayani Songea hadi Nyasa, kisha umeme utasambazwa ili kuondoa tatizo la uhakika wa nishati hiyo na hatimaye kuvutia wawekezaji zaidi.

Dk Samia ametoa ahadi hiyo leo, Jumapili Septemba 21, 2025 alipozungumza na wananchi wa Mbambabay, katika mkutano wake wa kampeni za urais, uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Sambamba na kituo hicho cha kupoza umeme, amesema pia wilayani Nyasa kutafungwa mtambo wa kukaushia samaki na kukoboa kahawa ili kuongeza ajira kwa vijana.

Mradi huo, amesema utaambatana na hatua ya Serikali kufikiria mpango wa ujenzi wa soko la kimataifa, ili kukuza mapato na kuwaongezea fursa wananchi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments