Kocha Msaidizi wa Mlandege FC, Hassan Ramadhan, amesema kikosi chake kilishindwa kuhimili baridi kali ya Ethiopia na hivyo kupoteza 2-0 dhidi ya Ethiopia Insurance katika Klabu Bingwa Afrika.
Amesema wanarudi Zanzibar kujiandaa kwa mchezo wa marudiano, wakiahidi kutumia faida ya uwanja wa nyumbani kusaka ushindi wa kusonga mbele.