Wednesday, December 10, 2025
spot_img
HomeHabariWamasai Ngorongoro waonesha imani kwa CCM na Rais Samia

Wamasai Ngorongoro waonesha imani kwa CCM na Rais Samia

Jamii za kifugaji za Kimasai wilayani Ngorongoro zimeonesha imani kubwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, wakitarajia suluhisho la kudumu kwa changamoto ya malisho kupitia Tume ya Serikali iliyoundwa kuchunguza masuala ya Hifadhi ya Ngorongoro na Pori Tengefu la Pololeti.

Katika mikutano ya kampeni za mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Ngorongoro, Yanick Ndoinyo, iliyofanyika katika kata za Oloipiri, Suitsambu na Oloolosokwan, viongozi wa jamii pamoja na wagombea wa chama hicho walisema wako tayari kumpa kura Rais Samia katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, wakiamini ataweka suluhisho thabiti la changamoto zinazowakabili.

Wagombea udiwani wa CCM, Latajewo Sayori (Oloipiri) na Methew Mollel (Ololosokwan), walisema serikali mpya itakayoongozwa na Rais Samia itaendeleza mshikamano wa kijamii na kuhakikisha rasilimali za wananchi zinasimamiwa kwa ufanisi zaidi.

Kwa upande wake, mgombea ubunge Ndoinyo aliwataka wananchi kumpigia kura Rais Samia kwa wingi, akibainisha kuwa serikali ya CCM ikishika hatamu kwa miaka mitano ijayo, wananchi wataweza kukuza biashara, kupunguza utegemezi wa ufugaji pekee na kuongeza fursa za maendeleo.

Wananchi wa Ngorongoro sasa wamesema wana matumaini kuwa kura yao kwa CCM itakuwa daraja la kufungua ukurasa mpya wa maendeleo, uhifadhi wa mazingira na ustawi wa jamii.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments