Monday, December 15, 2025
spot_img
HomeMichezoKocha Maximo: Safu ya ushambuliaji yatugharimu

Kocha Maximo: Safu ya ushambuliaji yatugharimu

Kocha wa KMC, Mbrazili Marcio Maximo amesema kichapo cha bao 1-0 walichopata dhidi ya Singida Black Stars kimesababishwa na udhaifu wa safu ya ushambuliaji iliyoshindwa kutumia nafasi nyingi zilizopatikana.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Maximo alisema licha ya kupoteza, anafarijika kuona wachezaji wake wakipambana na anaamini wataendelea kukua kadri msimu unavyosonga. “Ni hatua kwa hatua, wachezaji ni wadogo na wanahitaji muda wa kukuzwa,” alisema.

Kocha huyo amewataka wachezaji kusahau matokeo hayo na kuelekeza nguvu kwenye mechi zijazo, akisisitiza safari bado ni ndefu. KMC ilikuwa imeanza msimu vizuri kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji Septemba 17, lililofungwa na Daruweshi Saliboko.

Hii ni mara ya tatu kwa Maximo kufundisha nchini, baada ya kuinoa Taifa Stars (2006-2010) na Yanga (2014). Pia ndiye aliyeiongoza Stars kufuzu CHAN kwa mara ya kwanza mwaka 2009.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments