Tuesday, December 16, 2025
spot_img
HomeMichezoSongea United yatambulisha kikosi cha wachezaji 27

Songea United yatambulisha kikosi cha wachezaji 27

Songea United imetangaza kikosi cha wachezaji 27 kuelekea msimu mpya wa Ligi ya Championship unaoanza Oktoba 10.

Klabu hiyo imesajili wachezaji wapya 17 wakiwemo Bosco Magoli (Kagera Sugar), Amos Chilambo (Nyumbu), na Stanley Deodatus (Biashara United), huku nyota wa zamani 10 wakiendelea kubaki kikosini.

Songea United itaanza msimu kwa kuikaribisha Stand United ya Shinyanga Oktoba 11 kwenye Uwanja wa Majimaji, Ruvuma.

Michezo mingine ya ufunguzi itawakutanisha Kagera Sugar dhidi ya Transit Camp Kaitaba, na Mbuni FC dhidi ya Mbeya Kwanza jijini Arusha.

Ligi hiyo itatoa timu mbili zitakazopanda moja kwa moja Ligi Kuu msimu wa 2026/2027.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments