Sunday, December 7, 2025
spot_img
HomeHabariDkt Samia: Nitaimarisha maendeleo, kukuza uchumi

Dkt Samia: Nitaimarisha maendeleo, kukuza uchumi

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema dhamira ya Serikali yake katika miaka mitano ijayo ni kuimarisha maendeleo ya jamii, yanayohusisha sekta za afya, elimu, maji safi na nishati.

Dkt Samia ameyasema hayo leo, Jumanne Oktoba 7, 2025 alipozungumza na wananchi wa Sengerema mkoani Mwanza, katika mkutano wake wa kampeni za urais.

Amesema ni bahati nzuri Serikali yake, imefanya makubwa na mazuri kwenye sekta hizo, hadi sasa wananchi wanajivunia.

Mengina atakayofanya, amesema ni kuendelea uchumi, kwa kuhusisha sekta za kilimo, uvuvi, ufugaji, madini na nyingine zote za uzalishaji.

“Ndio maana kwenye kilimo, ufugaji na uvuvi, Serikali tumejitoa kutoa ruzuku nyingi ili sekta hizi zikue zilete ajira, mapato kwa watu wetu, zilete ustawi wa maisha ya watu wetu,” amesema.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments