Sunday, December 7, 2025
spot_img
HomeHabariSamia: Ole wao wanaopanga vurugu Oktoba 29

Samia: Ole wao wanaopanga vurugu Oktoba 29

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Samia Suluhu Hassan amewahakikishia Watanzania kuwa, hakuna atakayeruhusiwa kuthubutu kuvuruga amani siku ya uchaguzi, akisisitiza Serikali imejipanga kukabili vitendo hivyo.

Katika msisitizo wake kuhusu hakikisho hilo, Dk Samia amesema atakayethubutu hata kupasua kile alichokiita kibati, mamlaka zitashughulika naye kwa kadiri inavyopaswa.

Hili ni hakikisho la pili la usalama na amani siku ya uchaguzi wa Oktoba 29, linalotolewa na Dk Samia, baada ya awali kuweka msisitizo wa kutoruhusu aina yoyote ya uvunjifu wa amani, hivyo wananchi wajitokeze kupiga kura bila woga.

Dk Samia ametoa kauli hiyo leo, Ijumaa Oktoba 10, 2025 alipozungumza Bariadi Mjini, mkoani Simiyu, katika mkutano wake wa kampeni za urais, uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Amesema anatambua kuna watu wanajaribu kuwatisha wananchi wasijitokeze kupiga kura, akiwahakikishia Watanzania wasiogope kwa kuwa tayari Serikali imejipanga vema kumkabili yeyote atakayethubutu kuwabughudhi wapiga kura.

“Kuna watu wanatishatisha ili kuwafanya watu wasitoke Oktoba 29. Nataka kuwaambia ninayezungumza hapa ni Amiri Jeshi Mkuu wa Nchi hii. Nataka kuwaambia wasithubutu kibati tu kikipasuka, sisi tuko nao, tumejipanga vizuri,” amesema.

Amesema Serikali imejipanga vema wananchi wakapige kura na kurudi nyumbani kupumzika, wasipate hofu wala wasiogope.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments