Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene, amemwagia sifa Waziri Mkuu mpya, Dk. Mwigulu Lameck Nchemba, kuwa ni mbobevu kwenye uongozi.
Aidha, amesema umri wake wa miaka 50 unaweza kubeba kila rika la anaowaongoza hasa kundi la vijana wengi ambao ni wabunge waliopo bungeni.
Nchemba ameteuliwa leo Novemba 13, 2025 na Rais Samia Suluhu Hassan na kisha bunge kumpigia kura ya kumthibitisha kushika nafasi hiyo.




