Friday, December 5, 2025
spot_img
HomeMichezoSerikali kuanzisha ujenzi wa bwawa la kisasa la kuogelea

Serikali kuanzisha ujenzi wa bwawa la kisasa la kuogelea

Serikali imepanga kujenga bwawa la kuogelea la kisasa lenye urefu wa mita 50 ili kuimarisha na kukuza mchezo huo nchini. Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Boniface Tamba, wakati wa kufunga kongamano la kuendeleza mchezo wa kuogelea lililofanyika PSSSF Tower jijini Dar es Salaam.

Tamba alisema kongamano hilo limeibua hoja muhimu, ikiwamo ukosefu wa bwawa kubwa la viwango vya kimataifa, na kwamba serikali inalishughulikia suala hilo kwa haraka.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Prime Sports Agency, Lameck Borega, waliokuwa wadhamini wakuu wa kongamano hilo, alisema wamefurahishwa na uamuzi wa serikali kwani kwa sasa wanategemea mabwawa binafsi.

Rais wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA), David Mwasyoge, alisema kongamano hilo limewakutanisha wadau kutoka nchi mbalimbali na kujadili mbinu za kukuza mchezo huo, hasa ikizingatiwa Tanzania ina waogeleaji 250 pekee katika mikoa 26.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments