Monday, December 8, 2025
spot_img
HomeHabariDk Samia: Sitachoka kunyoosha tena mkono wa maridhiano

Dk Samia: Sitachoka kunyoosha tena mkono wa maridhiano

Rais Samia Suluhu Hassan amesema ingawa dhamira yake ya maridhiano wakati wa muhula wake wa kwanza wa uongozi ilikatishwa na baadhi ya wadau, katika awamu hii hatachoka kunyoosha tena mkono wa kufanikisha hilo.

Katika muhula huo, Rais Samia amesema alikuja na falsafa ya R4 ili kuliunganisha Taifa. Serikali ilionyesha utayari wakati wote kuleta maridhiano ili kwa pamoja kulijenga na kulitunza Taifa.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo, Ijumaa Novemba 14, 2025 alipozungumza wakati wa hotuba yake ya kulifungua bunge la 13, jijini Dodoma.

“Katika muhula wa kwanza wa awamu ya sita, tulikuja na falsafa ya R4 ili kuliunganisha Taifa. Serikali ilionyesha utayari wakati wote kuleta maridhiano ili kwa pamoja tujenge na kulitunza Taifa letu.

“Serikali ilinyoosha mkono na kuwakaribisha vyama vya siasa, sekta binafsi n ahata jumuiya za kimataifa ili kwa pamoja tuijenge Tanzania,” amesema.

Ameeleza mkono huo ulileta matumaini kwa nchi kabla ya baadhi ya wadau kuamua kuachilia au kuuputa mkono huo.

“Kwa kuwa wananchi wa Tanzania wamenipa ridhaa ya kuendelea kuiongoza nchi hii, sitachoka kunyoosha tena mkono wa maridhiano. Ni matumaini yangu kuwa wadau wa kisiasa wataupokea kwa dhati mkono wa maelewano ili kwa pamoja tujenge mazingira mwafaka kwa Taifa letu,” amesema.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments