Sunday, December 7, 2025
spot_img
HomeHabariAAFP: ACT jiungeni na SUK

AAFP: ACT jiungeni na SUK

Mwenyekiti  wa Chama cha AAFP, ambaye pia alikuwa mgombea urais katika uchaguzi uliopita, Said Soud, ameitaka chama cha ACT Wazalendo kushirikiana katika serikali ya umoja wa kitaifa ili kuunga mkono jitihada za Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, katika kuendeleza umoja na utulivu wa kisiasa visiwani Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari akiwa katika Ofisi za Chama hicho Kianga nje ya Mji wa Zanzibar leo, Said Soud amesema kushirikiana kwa vyama vya siasa katika serikali ya umoja ni muhimu ili kuhakikisha maendeleo endelevu na ustawi wa wananchi. 

Amesisitiza kuwa Zanzibar inahitaji mshikamano wa kisiasa na kushirikiana bila kujali tofauti za kisiasa.

“Tunashauri ACT Wazalendo wajitokeze kushirikiana katika serikali ya umoja wa kitaifa. Hii itasaidia kuhakikisha kwamba mpango wa maendeleo unaoongozwa na Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi unaendelea bila vizuizi vya kisiasa,” alisema Soud.

Ameongeza kuwa ushirikiano huo utakuwa kielelezo cha kuonyesha kuwa maslahi ya taifa ni mbele ya maslahi ya vyama, na kwamba viongozi wanapaswa kuweka kipaumbele huduma kwa wananchi badala ya mizozo isiyo na tija.

Aidha, Soud aliahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, huku akisisitiza kwamba maendeleo ya Zanzibar yanahitaji mshikamano wa kisiasa na ushirikiano wa vyama vyote vya siasa.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments