Akiba Benki yazindua kampeni “Tupo Mtaani Kwako” kibabe

Kaimu Afisa Mkuu wa Kitengo Biashara Benki ya Akiba, Danford Muyango.

Kaimu Afisa Mkuu wa Kitengo Biashara Benki ya Akiba, Danford Muyango amesema taasisi za kifedha hazina budi kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi kwa kuwasogezea karibu ili kusaidia kupunguza adha ya kutumia muda mwingi kufuata huduma umbali mrefu na kuchelewa kufanya shughuli zao za kiuchumi.

Kauli hiyo ameitoa leo Septemba 21, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati akizindua rasmi kampeni ya “Tupo Mtaani Kwako” katika tawi la Kijitonyama la benki hiyo, Letsya Tower.

Amesema Akiba Benki wapo mtaani kila mahali wakitoa huduma ikiwemo elimu ya mikopo, jinsi ya kutumia huduma za kidigital VISA card,ACB Mobile, Akiba Wakala na Internet Banking.

”Tumezindua rasmi program yetu ya TUPO MTAANI KWAKO kupitia timu yetu bobezi ya mauzo sasa tunakufika popote ulipo nchi nzima kupitia timu yetu ya mauzo kupata huduma zetu za kufungua akaunti , elimu ya mikopo pamoja na jinsi ya kutumia huduma zetu za kidijitali za VISA card, ACB Mobile, Akiba Wakala na Internet Banking” amesema

Ameongeza kuwa Program hiyo inaenda sambamba na kampeni ya Road show ya kutoa utambulisho kwa timu ya “Tupo Mtaani kwako” katika vitongoji na mitaa mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *