Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, amesema alitarajia upinzani mkali dhidi ya Dodoma Jiji FC baada ya mchezo wa sare ya bila kufungana uliopigwa jijini Dodoma.
Barker ameeleza kuwa hakuingia uwanjani kwa kubeza uwezo wa wapinzani wake, akitambua kazi nzuri inayofanywa na kocha Amani Josiah tangu alipoichukua timu hiyo.
“Nimewahi kuzungumza na Amani Josiah kuhusu ubora wa kikosi chake, na nilijua wazi kuwa mechi dhidi ya Dodoma Jiji ingekuwa ngumu. Tangu awe chini ya Josiah, timu imekuwa imara na yenye ushindani mkubwa,” amesema Barker.
Hata hivyo, kocha huyo ameongeza kuwa anasikitishwa na matokeo hayo, akieleza kuwa wachezaji wake walijituma na kufanya kila walichopaswa kufanya, lakini walishindwa kupata bao la ushindi.




