Kocha Mkuu wa Coastal Union, Ally Ameir, amesema msimu ujao timu yake itakuwa tishio kupitia mabao ya faulo kutokana na mazoezi maalum waliyoyafanya.
Ameir alisema tayari wachezaji wameanza kufunga mabao kwa njia hiyo, mfano ukiwa ni mchezo wa kirafiki dhidi ya Fountain Gate ambapo mabao yote yalifungwa kupitia mipira iliyokufa.
Aliongeza kuwa maandalizi yanaendelea vizuri, akibaini makosa ya kiufundi katika mechi za kirafiki na kuyarekebisha.
Jumapili hii Coastal itapambana na APS Bomet ya Kenya kwenye Coastal Festival.




