Baada ya kushinda 1-0 dhidi ya Prisons kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu, Coastal Union leo itakipiga na JKT Tanzania katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Kocha Mkuu, Ally Ameir, amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi akiahidi kuwapa burudani nyingine, huku nahodha Bakari Msimu akisema morali ya wachezaji iko juu na wamefanyia kazi makosa ya mchezo uliopita.