Thursday, December 18, 2025
spot_img
HomeAfyaDC Korogwe awataka wadau wa afya Tanga, kuimarisha usimamizi wa bidhaa za...

DC Korogwe awataka wadau wa afya Tanga, kuimarisha usimamizi wa bidhaa za afya

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe William Mwakilema amewataka wadau na wasimamizi wa sekta ya afya Mkoani Tanga, kuimarisha usimamizi wa bidhaa za afya kwenye maeneo yao ya kazi, ili wananchi wapate huduma bora bila changamoto.

Mwakilema ametoa rai hiyo hii Leo wakati akifungua kikao cha wateja na wadau wa MSD kanda ya Tanga, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, waliokutana Wilayani Korogwe kwa ajili ya kujadili namna bora ya kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya mkoani humo.

“Ni wajibu wenu kuhakikisha hakuna upotevu wa dawa na vituo vyote vinakusanya mapato, ili kuilipa MSD kwa wakati, lengo likiwa ni kuiongezea msuli wa kuhakikisha bidhaa za afya zinapatikana wakati wote” alisema Mwakilema

Katika hatua nyingine, amebainisha umuhimu wa vituo vya kutolea huduma za afya kukusanya mapato na kulipa madeni kwa MSD kwa wakati, kufanya maoteo sahihi ya mahitaji ya dawa, na kusimamia matumizi ya takwimu katika maamuzi.

Mwakilema amesisitiza kwamba Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeongeza bajeti ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba maradufu, hivyo ni wajibu kwa watendaji hao kuhakikisha zinatumika ipasavyo kama ilivyo kusudiwa bila upotevu au kuchepushwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Ugavi na Uendeshaji wa MSD, Victor Sungusia, amesema MSD inaendelea kuboresha utendaji kazi wake, kwa kuhakikisha huduma zinapatikana kwa wakati, sambamba kukidhi mahitaji ya wateja hali ambayo imeimarika siku hadi siku, ukilinganisha na kipindi cha nyuma.

Sungusia amewataka washiriki hao kutoa mrejesho wa huduma na maoni yao kwa uwazi, ili kuisaidia MSD iweze kuboresha huduma zake zaidi, kwani mchango wao ni muhimu katika ukuaji wa MSD.

Naye Kaimu Meneja wa MSD Kanda ya Tanga Grants Mwapele, amedokeza kwamba MSD Tanga imeboresha huduma zake, ikiwemo upatikanaji wa bidhaa za afya, ambao umepanda kutoka asilimia 51 katika mwaka wa fedha 2023/24 hadi kufikia asilimia 75, huku wakitarajia kufikia asilimia 90 katika mwaka huu wa fedha 2025/26.

Mwapwele amewashukuru wateja na wadau hao kwa kuendelea kuiunga mkono MSD, huku akiwasihi kuendelea kushirikiana kwa ukaribu, ili kuondokana na changamoto chache zilizosalia na kuimarisha huduma za MSD mkoani humo.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments