Tuesday, December 16, 2025
spot_img
HomeHabariDCI amuita Polepole kujibu tuhuma dhidi ya serikali

DCI amuita Polepole kujibu tuhuma dhidi ya serikali

Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) imemtaka aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, kufika ofisini hapo kutoa maelezo na ushahidi kuhusiana na tuhuma ambazo amekuwa akizitoa kwa umma kupitia mitandao ya kijamii.

Polepole alijiuzulu wadhifa wake mnamo Julai 13, 2025 akieleza kuwa hawezi kuendelea kuwa sehemu ya uongozi usiohamasika na usiofuata misingi ya katiba ya nchi na chama, pamoja na haki, maadili, utu na uwajibikaji kwa wananchi.

Tangu kujiuzulu kwake, amekuwa akitoa kauli mbalimbali zenye kuibua tuhuma dhidi ya Serikali na taasisi zake.

Akizungumza leo Jumatatu, Septemba 15, 2025, Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime, alisema kuwa jeshi hilo limefungua jalada la uchunguzi na linaendelea kuchunguza tuhuma hizo, huku likimtaka Polepole kushirikiana kwa kutoa maelezo na vielelezo vinavyohitajika.

Hatua hii ya DCI inatajwa kuwa sehemu ya mchakato wa kisheria na kikanuni wa kufuatilia madai yote yanayohusu taasisi za Serikali na viongozi wake, ili kuhakikisha ukweli unabainika na kulinda maslahi ya taifa.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments