Tuesday, December 16, 2025
spot_img
HomeHabariDk. Samia aahidi huduma bora kwa wananchi

Dk. Samia aahidi huduma bora kwa wananchi

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Samia Suluhu Hassan amesema katika kipindi cha miaka mitano ijayo, Serikali yake itaendelea kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote za jamii, kwa kuwa ni wajibu wa msingi.

Dk Samia ameyasema hayo leo, Jumanne Septemba 23, 2025 alipozungumza na wananchi wa Masasi mkoani Mtwara, wakati wa mkutano wake wa kampeni, uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Ameahidi Serikali yake katika kipindi hicho itaendelea kutoa huduma kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote za jamii ikiwemo maji, umeme na vituo vya afya.

“Hiyo kwa Serikali ni kazi ya kawaida, wala hatusemi ni kazi ya maendeleo, ni kazi ya kawaida ni kazi yetu. Kazi za maendeleo ni ujenzi wa barabara, bandari na mambo kama hayo,” amesema.

Sambamba na hilo, amesema ataanzisha mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) mkoani humo, ili kuiunganisha Bandari ya Mtwara na Mbambabay mkoani Ruvuma.

“Ndani ya miaka mitano tukifanikiwa huo ndiyo mradi mwingine mkubwa unaokuja hapa Mtwara na nikifika Lindi nitawaambia mradi wao mkubwa ambao tupo katika hatua za mwisho, ukifika muda tutawaambia,” amesema Dk Samia.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments