Sunday, December 7, 2025
spot_img
HomeHabariDk. Samia: CCM vyetu ni vitendo

Dk. Samia: CCM vyetu ni vitendo

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Samia Suluhu Hassan amesema Serikali za chama hicho, zimejikita katika kutenda zaidi, badala ya maneno.

Dk. Samia ameyasema hayo leo, Jumamosi Septemba 20, 2025 alipozungumza na wananchi wa Pemba visiwani Zanzibar katika mkutano wake wa kampeni za urais.

“Waswahili wanasema ada ya mja kunena, waungwana vyao ni vitendo. Serikali za CCM, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar, sisi vyetu ni vitendo na wala sio blaa blaa… sisi vyetu ni vitendo,” amesema.

Uthibitisho wa hilo, amesema ni namna Serikali hizo zilivyofanya kazi kubwa ya kusimamia na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ushirikiano wa pande zote mbili.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments