Rais Samia Suluhu Hassan amesema tayari ameshaielekeza Wizara ya Afya kusimamia maelekezo ya kutozuia maiti kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, wakati familia zikiendelea na taratibu za kulipa deni la gharama za matibabu zinazolinda utu wao.
Hata hivyo, amesema kupitia mpango wa bima ya afya kwa wote, kadhia hiyo itakomeshwa kwa kuwa gharama za matibabu zitalipwa na bima ya anayekwenda kutibiwa, hivyo wananchi wahakikishe wanakuwa na bima hiyo.
Rais Samia ameeleza hayo leo, Ijumaa Novemba 14, 2025 alipozungumza katika hotuba yake ya kulifungua Bunge la 13, jijini Dodoma.




