Rais Samia Suluhu Hassan amesema ana imani na matumaini makubwa na Tume aliyoiunda ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani ya Oktoba 29, mwaka huu na kwamba itatenda haki.
“Jana nilikuwa nasoma article fulani, wenzetu wapinzani wanasema hawana imani na tume yoyote ya ndani, wanataka tume itoke UN, AU itoke Umoja wa Ulaya ndio ije ifanye kazi hapa Tanzania,” amesema.
Amesema imani aliyonayo inatokana na ubobezi na uzoefu walionao wajumbe aliowateuwa kuiongoza tume hiyo na anaamini mapendekezo yatalitoa Taifa lilipo na kulisogeza mbele.
Hata hivyo, amesema mapendekezo ya tume hiyo ndiyo yatakayokuwa ajenda za tume ya maridhiano aliyoahidi kuiunda ndani ya siku 100 za uongozi wake.
Rais Samia ametoa kauli hiyo leo, Alhamisi Novemba 20, 2025 alipozungumza wakati wa uzinduzi wa Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.




