Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan ameahidi kuanzisha kituo cha kumbukumbu na nyaraka za muungano, ambacho ndani yake wageni na vizazi vijavyo, viytajifunza kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Amesema muungano huo, ulioasisiwa na Baba wa Taifa, Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume, umeimarika na sasa Tanganyika na Zanzibar zimefungamana kifamilia, kibiashara, kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Ameeleza miongoni mwa mambo ambayo Serikali yake inajivunia ni kuudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Dkt Samia ametoa ahadi hiyo leo, Jumatano Septemba 17, 2025 alipozungumza na wananchi wa Makunduchi, visiwani Zanzibar katika mkutano wake wa kampeni za urais.




