Mgombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema miradi mbalimbali iliyokuwa inatekelezwa visiwani Zanzibar, ndiyo iliyosababisha maeneo mengi yazungushiwe mabati.
Amesema hatua hiyo imesababisha Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi apachikwe jina la ‘Mzee wa Mabati’ lakini sasa yameondolewa na miradi mbalimbali inaonekana.
Dkt Samia ameyasema hayo leo, Jumatano Septemba 17, 2025 alipozungumza katika mkutano wa kampeni za urais, Makunduchi, visiwani Zanzibar.




