Thursday, December 18, 2025
spot_img
HomeHabariDk. Samia:Mwendo utakuwa uleule kuboresha huduma za jamii, kukidhi mahitaji

Dk. Samia:Mwendo utakuwa uleule kuboresha huduma za jamii, kukidhi mahitaji

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Serikali atakayoiunda itaendelea kuboresha sekta za maendeleo ya kijamii zikiwemo za elimu,umeme,maji na afya ili kukidhi mahitaji ya wananchi wanaongoza kila kukicha wanaongezeka katika maeneo mbalimbali.

Dkt Samia amewahakikishia kuwa Serikali itakuwa na mwendo ule ule katika kuboresha huduma hizo kwa Watanzania, kama ilivyofanya kuanzia mwaka 2021 wakati alipoingia madarakani.

“Tunajhua jinsi Watoto na vijana wetu wanavyokua, mahitaji haya yanaongezeka. Itafika mahali tutamaliza haja ya umeme, pindi tutakapounganisha vitongoji vyote na kitakachobaki ni kuunganisha kwenye makazi ya wananchi,”

“Kwenye maji tunajua jinsi watu wanavyongezeka, mahitaji yanakuwa, tutaendelea kutoa mahitaji,vivyo hivyo hivyo kwenye afya na elimu pia.Tutaendelea kujenga madarasa ya sekondari na msingi, sambamba na ujenzi wa vyuo vya Veta ili kuwapa vijana wetu ujuzi, kubwa Zaidi tunakusudia kuweka viwanda vidogo vidogo vitakavyoongeza thamani mazao kwenye wilaya husika na kutengeza ajira,” amesema Dkt Samia.

Dkt Samia ameeleza hayo leo Alhamisi Septemba 11,2025 wakati akihutubia mkutano wa kampeni za kusaka kura za uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, katika wilaya ya Uyui mkoani Tabora ambapo atakuwa kwa siku tatu kujinadi na kueleza atakayoyafanya endapo atapata ridhaa ya kuongoza kwa miaka mitano ijayo.

Aahidi neema Uyui

Katika mkutano Dkt Samia amewaahidi wananchi wa Uyui, akisema ahadi kuwaajiri watumishi wa elimu 7000 na watumishi wa kada ya afya 5000, miongoni mwao watapelekwa wilayani humo ili kutoa huduma.

“Niliahidi ndani siku 100, mkinipa ridhaa ya kuongoza nchi tutaajiri 5000 bila shaka watafika hapa (Uyui). Lakini katika sekta ya elimu watumishi 7000 wengine watafika hapa,” amesema Dkt Samia huku akishangiliwa na wananchi wa Uyui yenye majimbo mawili ya Igalula na Uyui yenyewe.

Katika hatua nyingine, Dk Samia amesema barabara za Ilolanguru -Isenga hadi Kasisi A na Ndono Mfuluma hadi Makazi zilipo wilayani Uyui zitakwenda kujengwa ili zipitike vizuri.Pia aliahidi kulibeba ombi la mbunge wa jimbo kuhusu ujenzi wa barabara kutoka Kahama hadi Tabora.

Wakulima tumbaku mtalipwa

Dkt Samia amewahakikishia kuwa Serikali bado inaendelea na mazungumzo na kampuni zinazohusika na masuala hayo, ili kuhakikisha fedha wanazodaiwa na wakulima zinalipwa.

“Kupitia Waziri wa Kilimo (Husseni Bashe), huwa nataka ripoti kila baada ya muda, aniambie mazungumzo yamefikia wapi ili wakulima walipwe fedha zao,” amesema Dkt Samia.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments